Jux atinga Coke Studio msimu mpya

0
210

Mwanamuziki wa Bongo fleva Juma Jux atakuwa mmoja wa washiriki wa shoo ya Coke Studio ambapo itashirikisha wasanii wakubwa kutoka bara la Afrika.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa msanii huyo kushiriki onesho hilo kwa msimu wa 2019 ambapo ataonyesha kipaji chake kwenye shindano hilo.

Jux amesema kuwa moja ya mipango yake kwa mwaka 2019 ni kufanya nyimbo nyingi za kushirikiana na wasanii kutoka nje ya Tanzania. Katika Coke Studio Jux anashirikiana na Shellsy Baronet kutoka Mozambique.

Kwenye interview yake aliyofanya Jux amefunguka mengi juu ya mara yake ya kwanza kushiriki kwenye msimu mpya wa Coke Studio.

Jux ataiwakilisha Tanzania katika jumba la Coke Studio kwa mwaka 2019, kuanzia Februari mwakani akiwa na wasanii wenzake kutoka mataifa mbali mbali ya Tanzania.

LEAVE A REPLY