Jux akataa kumuongelea vibaya Vanessa Mdee

0
235

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Juma Jux amesema kuwa hawezi kumuongelea vibaya aliyekuwa mpenzi wake wa zamani mwanamuziki, Vanessa Mdee hata kama wameachana.

Jux amesema kuwa licha ya kuachana kwao lakini bado yupo sawa na Vanessa Mdee pia hajamu ‘unfollow’ kupitia mitandao ya kijamii.

Jux amesema kuwa “Sioni sababu ya kumongelea vitu vibaya na kwanini nifanye hivyo na nisiongee vitu vizuri wakati alikuwa mtu wangu wa karibu”.

Pia Jux amesema kuwa kwenye vitu vibaya na vizuri huwa nachagua vizuri siku zote, hayo ni maamuzi ya mtu au malezi ya mtu kwa sababu nimeshakuwa katika matukio mazuri na yeye kipindi cha nyuma na zilikuwa bora zaidi kuliko kipindi hiki” amesema Jux.

Jux na Vanessa Mdee wameachana miezi kadhaa iliyopita, ambapo sasa hivi kila mtu yupo katika mahusiano mapya.

LEAVE A REPLY