Jux akanusha madai ya Chid Benz

0
338
Jux

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Jux amesema kuwa amesikitishwa na kauli ya Chid Benz kuwa alifanya show ya ‘In Love & Money bila kulipwa na msanii huyo.

Chid Benz alitumbuiza katika show ya ‘In Love & Money’ iliyoandaliwa na Jux pamoja na mwanamuziki Vanessa Mdee miezi miwili nyuma.

Jux amesema Chid Benz hakuwa kwenye listi ya wasanii wanaotumbuiza katika tamasha hilo, zaidi alimfuata ‘backstage wakati wa show ikiendelea na kumuomba kutumbuiza.

Kuhusiana na hali ya msanii Chid Benz ilivyo kwasasa, Jux amesema anasikitishwa kumuona msanii huyo akitumiwa katika mambo maovu ambayo hayawezi kumjenga kimaendeleo badala yake imekuwa ni utani unaoendelea kuwafurahisha mashabiki.

Jux anajipanga kuja na album yake mpya kwa mara ya kwanza, itakayoenda kwa jina la ‘IN LOVE’ anayopanga kuiachia mwakani.

LEAVE A REPLY