Jux akanusha kutokana kimapenzi na Huddah Monroe

0
66

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Juma Jux amekanusha kutoka kimapenzi na mrembo kutoka nchini Kenya Huddah Monroe tofauti na watu wanavyosema.

Msanii huyo amesema hayo baada ya tetesi kusambaa kuwa anatoka kimapenzi na mrembo huyo kutoka Kenya jambo ambalo halina ukweli.

Jux amesema kuwa habari hizo sio za kweli licha ya kuwa mrembo huyo ana vigezo vyote anavyovihitaji yeye.

“Ni msichana mrembo, ana asilimia kama themanini hivi ya vigezo ninavyovihitaji kwa mwanamke, lakini hiyo haifanyi mimi na yeye tukawa wapenzi, namheshimu kama dada yangu na tumekuwa tukishirikiana sana kwenye kazi, isitoshe Hudah ana mtu wake,” alisema Jux.

Jux amesema kwamba ameona watu wanavyosema mitandaoni kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mrembo huyo, jambo ambalo halina ukweli kwa sababu tayari msichana huyo ana mtu wake.

LEAVE A REPLY