Jux aitamani ndoa

0
55

Mwanamuziki wa Bongo Flevs, Juma Jux amevunja ukimya kuwa muda umefika kwa yeye kufunga ndoa kwani ameshamaliza ujana.

Jux amethibitisha kuwa na uwezo wa kumtunza mwanamke kwa kila kitu hivyo haoni sababu ya kumzuia yeye kuwa ndani ya ndoa.

“Mimi ni mwanaume imara ambaye nina uwezo kumuhudumia mwanamke maana kwangu atakula, atakunywa, atavaa na hata vitu vingine atapata.

Kuoa ni baraka kubwa hapa duniani na hicho ndicho kifuatacho,” anasema Jux ambaye baada ya kutengana na Vanessa Mdee aliangukia kwenye penzi la mrembo Nayika wa Thailand.

LEAVE A REPLY