Jux afungukia mjengo wake mpya

0
59

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Juma Jux amesema anapenda sana nyumba nzuri hivyo hata ule mjengo wake mpya anao-post Instagram anaona bado hajafikia nyumba ambayo anataka iwe ya ndoto zake.

Jux amesema mjengo wake wa sasa upo vizuri lakini bado anajaribu kujenga nyumba nyingine zaidi ya hiyo

Ameongeza kwa kusema kuwa “Ile bado sio nyumba ya ndoto yangu na ambayo nataka kuishi japo tunajaribu tu kidogo na Mungu katujaalia, pale nakaa ndiyo lakini sio nyumba ya ndoto yangu.

Pia amesema kuwa anapenda sana nyumba na vitu vizuri, bado anaendelea kupambana ili kufikia nyumba ambayo nataka niwe nayo.

LEAVE A REPLY