Jux afunguka alivyotoka kimapenzi na Wolper

0
85

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Jux aliwahi kuwa na mahusiano na msanii wa filamu Jacqueline Wolper kipindi cha nyuma, japo watu wengi walikuwa hawafahamu.

Jux ameeleza kipindi yupo kwenye mahusiano na staa huyo wa filamu, hawakuachana vizuri ndiyo maana hakuna ukaribu kati yao au hata kusapotiana kwenye kazi zao.

Jux amesema  “Kipindi cha nyuma nilikuwa naye, inategemea mahusiano yanapoishiaga kutokana na mazoea, kwa upande wangu haikuwa sawa sana, lakini nilielewa kutokana na maisha baadaye kila kitu kikawa sawa

Sasa hivi tuko poa yeye ana maisha yake na mimi nina maisha yangu, hatuna tatizo lolote ni vya muda sana hivi”.

“Kwani ni lazima anisapoti au awekewe lawama zote hizo, mimi sikasiriki kabisa na siangaliagi hivyo vitu, wafuasi ambao mimi ninao kwenye Instagram yangu, alionao Ben Pol au Wolper ni walewale tu.

LEAVE A REPLY