Juventus na Manchester United wafikia makubaliano ya awali

0
138
during the Serie A match between Juventus FC and AC Chievo Verona at Juventus Arena on January 25, 2015 in Turin, Italy.

Klabu ya Manchester United imekaribia zaidi kumnasa kiungo wake wa zamani anayechezea Juventus ya Italia, Pau Pogba baada ya kukubali kuongeza pesa kufuatia kukataliwa kwa dau la kwanza.

Manchester United waliiongeza pesa zaidi kwenye dau la kwanza la £87m siku Jumatano lakini wakurugenzi wa Juventus Giuseppe Marotta na Fabio Paratici walikataa tena.

United imelazimika kukubali kulipa dau la £92m moja kwa moja kwa Juventus kisha kulipa 20% ya gharama za wakala wa mchezaji huyo, Mino Raiola zinayoaminika kufikia £18.4m.

Mwanzoni Juventus walisema kuwa mchezaji huyo ataondoka kwa £100m lakini sasa wamekubali kumuuza kwa £92m kama United watakubali kulipa gharama za wakala wake.

Tayari United wameshakubaliana maslahi binafsi ya Pogba ikiwemo mshahara, haki za matangazo na ziada zitokanazo na ufanisi na mafanikio yake uwanjani.

Huenda Paul Pobga akafikisha mavuno yake hadi  £290,000 kwa wiki kutokana na haki mbalimbali huku malipo ya mshahara pekee yakifikia £220,000 kwa wiki.

Paul Pogba anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano na mashetani hao wekundu wa Manchester na kuwa mchezaji wan ne kusajiliwa na timu hiyo msimu huu na mchezaji wa mwisho kwenye orodha iliyopewa kipaumbele na kocha wa sasa wa United, Jose Mourinho.

Ingawa miamba hiyo ya Italia imekubaliana bei hiyo na Manchester United lakini bado haijatoa taarifa rasmi ya kuthibitisha kumuuza Paul Pogba.

LEAVE A REPLY