Jumba la Nicki Minaj lavamiwa na wezi, wasepa na vito vya £140,000 (TZS 390m)

0
325

Polisi katika jimbo la Los Angeles nchini Marekani wanapeleleza kesi nyingine ya kuibiwa kwa staa ikiwa ni miezi michache tangu staa wa Marekani, Kim Kardashian aporwe vitu vyake nchini Ufaransa.

Polisi katika jiji hilo kwa sasa wameanza uchunguzi kuhusiana na wizi uliofanyika kwenye jumba la staa Nicki Minaj ambapo vito vya thamani na mali nyingine zinazofikia £140,000 (TZS 390m).

Wizi huo umetokea kwenye jumba la staa huyo lililopo kwenye eneo la mastaa wa Marekani la Beverly Hills.

Polisi wa eneo hilo ambaop ndio waliotoa taarifa kwa vyombo vya habari wamedai kuwa inakadiriwa kuwa wizi huo umetokea kati ya terehe 24 Novemba mwaka jana na tarehe 24 Januari mwaka huu.

Hata hivyo Minaj amekataa kuzungumzia sakata hilo.

LEAVE A REPLY