Juma Nature na Chege wamaliza tofauti zao

0
95

Wasanii wakongwe wa Bongo Fleva, Juma Nature na Chege wamemaliza tofauti zao za muda mrefu baada ya wasanii hao kuamua kufanya kazi pamoja.

Kwa upande wake Nature amesema kwa sasa wao ni watu wazima na wajikita zaidi kufanya kazi na mashabiki wakae mkao wa kula na zamani sana kukaa na Chege na kufanya kazi, Sasa tumeshakuwa watu wazima na tunajitambua, tutapiga kazi, mashabiki wajiandae.”

Chege amesema ujio wao kwa sasa umeangalia zaidi nini soko linahitaji “Mimi na Chege tumeanza game kitambo watu wanatufahamu, lakini kutengeneza hii ngoma ya pamoja tumeangalia soko linataka nini, watu wametu-miss sana, lazima tufanye kitu wanachokitaka, hatuendi nje tunafanya kitu ambacho jamii wanakihitaji.”

Chege amesema kuwa Mimi ndio nilikuwa wa kwanza kumtafuta Nature miaka hiyo, niliona nikifanya kazi na huyu jamaa ipo siku nitakuja kutusua, nikapanga kolabo naye ikaleta ukaribu, Nature naye akaniona akaomba Management yake niende naye kwenye tour Uganda.”

Chege amesema kwa sasa hawezi kumzungumzia Temba ila wakati sahihi ukifika atalizungumzia”Siwezi kuzungumzia urejeo wa Kundi la TMK bali naweza kuzungumzia combination ya Chege na Nature.

Tuna mipango mingi ya kuifanya hii project ya Chege na Nature kuwa ya kipekee, hatutaiacha iwe nyepesi nyepesi, combination yetu itaacha alama.”

Menejimenti yangu imenizuia kuzungumzia masuala hayo, napaswa kuzungumzia project yangu na Nature, sio vizuri kuanza kuzungumzia watu kwa sasa, wakati wake ukifika tutazungumza.

LEAVE A REPLY