Joti ataka wasanii wakongwe waenziwe

0
89

Muigizaji wa vichekesho nchini, Joti ameiomba Serikali kuweka siku maalumu ya kuwaenzi waanzilishi wa Sanaa nchini ambao wameaga dunia.

Joti amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na wasanii nchini wanapaswa kuweka siku hiyo kwa ajili kuenzi mchango wao waliotoa katika jamii wakati walipokuwa hai hivyo ni vyema kuwakumbuka.

Joti alimtolea mfano marehemu Mzee Majuto ambapo amesema kuwa muigizaji huyo amewafanya vijana wengi kujiingiza kwenye tasnia ya uchekeshaji hivyo anafaa kuenziwa kwa mchango wake kwa jamii.

Pia Joti amemtolea mfano marehemu Max ambaye alikuwa muigizaji katika kundi la Kaole Sanaa Group ni waigzaji ambao waliinyanyua sanaa mpaka kufika hapa ilipo.

Mugizaji huyo wiki hii amezindua Tamthilia yake inayoitwa ‘Mwantumu’ msimu wa pili ambayo inaonyeshwa kupitia DSTV.

LEAVE A REPLY