Johari akiri mahaba yake kwa pombe

0
85

Muigizaji wa Bongo Movie, Johari Chagula amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake kitu kikubwa ambacho kimekuwa cha starehe kwake ni kunywa pombe na wala sio kitu kingine.

Mwanadada huyo ambae aliwahi kuripotiwa hata kuibiwa akiwa baa amelewa anakiri kuwa starehe yake kubwa kwa sasa ni pombe na sio kitu kingine.

Akiongea na waandishi wa habari, johari anasema kuwa  aliamua kuchaguwa pombe kuwa starehe na rafiki yake mkubwa kwa sasa akiwa amekunywa pombe hakuna shida na mtu anayosababisha.

Muigizaji ameweka wazi mapenzi yake kwenye pombe kwani kwa upande wake hana starehe yoyote zaidi ya kunywa pombe tu.

Muigizaji huyo amejipatia umaarufu kwenye fani ya uigizaji kutokana na ubora wake wa kushiriki kwenye movie anazoshiriki.

LEAVE A REPLY