Joh Makini atambulisha lebo yake ya muziki

0
45

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Joh Makini ametambulisha label yake ya muziki iitwayo Makini Record pamoja na kumtambulisha msanii mpya Otuck William.

Joh Makini ambaye anawakilisha kundi la Weusi amesema amekuja na label hiyo ili kusaidia vipaji vipya viweze kujilikana kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo.

Amesema kwa muda mrefu alikuwa anatamani kufanya hivyo lakini alikuwa anashindwa kutokana na mtaji wa kuwekeza ambapo kwa sasa amesema yupo tayari kuwasaidia wasanii wenye vipaji.

Joh Makini amewata mashabiki wake kuisapoti lebo hiyo ili kusaidia vipaji vya wasanii wa Bongo na kukuza muziki wa Bongo Fleva pamoja na muziki wa Hip Hop.

Lebo hiyo tayari ina mwanamuziki mmoja aliyetambulishwa na msanii huyo hivyo watakuwa wanatambulisha wasanii wapya ambao watakaokuwa wanakidhi vigezo.

LEAVE A REPLY