JLO aomba ulinzi wa Mahakama kutokana na mhalifu anayemfuatilia ‘kimyakimya’

0
170
PASADENA, CA - JANUARY 13: Actress Jennifer Lopez arrives at the 2016 Winter TCA Tour - NBCUniversal Press Tour at Langham Hotel on January 13, 2016 in Pasadena, California. (Photo by Angela Weiss/Getty Images)

Staa wa Marekani, Jennifer Lopez a.k.a JLO ameomba msaada wa Mahakama ya jiji la Los Angeles uweze kumlinda dhidi ya jamaa aitwaye Timothy McLanahan ambaye amekuwa akimfuatilia kwa muda mrefu.

McLanahan anayedaiwa kuwa na rekodi za uhalifu wa kutumia silaha na kufanya vurugu amekuwa akimfuatilia Lopez ‘kimyakimya’ kiasi kilichomtia hofu staa huyo wa Pop.

Kwenye maelezo aliyoyapeleka mahakamani JLO amedai kuwa McLanahan amekuwa akimfuatilia kwenye miji mbalimbali ikiwemo Los Angeles na Las Vegas na pia amekuwa akihudhuria maonyesho ya mwanamuziki huyo.

Lakini kilichomtisha zaidi JLO ni kuwa McLanahan amekuwa kituma maua na barua pepe na mbaya zaidi aliwahi kuvamia nyumba ya JLO iliyopo Las Vegas kabla ya kukamatwa na walinzi .

Baada ya JLO kudai anahofia usalama wake na watoto wake mapacha, Mahakama imemuamuru McLanahan kukaa pasipo kificho kwuanzia umbali wa yadi 100 kati yake na familia ya JLO.

LEAVE A REPLY