Jim Carrey ashtakiwa kwa kuhusika na kifo cha mpenzi wake

0
179

Staa wa filamu za vichekesho wa Hollywood, Jim Carrey amefunguliwa mashtaka ya kuhusika na kifo cha mpenzi wake wa zamani ambaye alifariki mwaka jana kwa kutumia kiasi kikubwa cha dawa.

Nyaraka za mahakama zinaonyesha kuwa Jim Carrey amefunguliwa mashtaka hayo kwa kutuhumiwa kuchukua dawa, ambazo zilitumiwa na mwanamke huyo Cathriona White kabla ya kifo chake, kwa kutumia jina la bandia.

Jalada la kesi hiyo iliyofunguliwa kwenye mahakama ya juu ya Los Angeles, inadai kuwa Jim Carrey alitumia jina la ‘Arthur King’ kujipatia dawa hizo.

Mume wa zamani wa mwanamke huyo, Mark Burton amesema kuwa staa huyo alitumia utajiri mkubwa alionao pamoja na umaarufu wake kupata dawa kwa njia ya udanganyifu.

Pamoja na shtaka hilo, Carrey anatuhumiwa pia kuficha ushiriki wake kwenye kifo cha mwanamke huyo.

Cathriona White alikutwa amefariki dunia kwa kutumia kiasi kikubwa cha dawa zikiwemo Ambien, Propranolol na Percocet.

Ripoti za wakati huo kabla ya kifo cha mwanamke huyo zilidai kuwa uhusiano wa wawili hao ulikuwa ukivunjika na kuimarika mara kwa mara na siku chache kabla ya kifo cha mwanamke huyo wawili hao waliripotiwa kuwa wameachana.

Pia, Bw. Burton anamtuhumu Carrey kwa kutuma meseji ya uongo ‘bogus message’ kwa White, siku moja kabla ya mwili wake kupatikana ili kuhadaa jamii juu ya kuhusika kwake na kifo hicho.

Msiba: Jim Carrey akita ameshiriki kebab genes la mpenzi wake White
Msiba: Jim Carrey akita ameshiriki kubeba jeneza la mpenzi wake Cathriona White

LEAVE A REPLY