Jide amtabilia makubwa Zuchu

0
111

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lady Jaydee amesema kuwa msanii mpya wa Lebo ya Wasafi Classic, Zuchu atafika mbali kutokana na juhudi zake.

Jide amesema kuwa Zuchu amekuwa na juhudi ya kutaka kukutana na watu waliotangulia ili kujifunza na hicho ndicho kitamfikisha mbali.

“Zuchu ana juhudi za kuwa karibu na watu waliomtangulia kwenye gemu, hii itamfanya kufika mbali zaidi na anajitahidi hata kwenye kazi zake.

Pia amesema kuwa kama sisi zamani tulikuwa tunawaongelea wanamuziki kama mama yake mzazi (Malkia Khadija Kopa), hiyo ni nzuri sana,’’.

LEAVE A REPLY