Jeshi la polisi nchini lafanya operesheni kali jijini Dar es Salaam

0
147

Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limekamata watuhumiwa sugu 1,066 kwa makosa mbali mbali ya unyang’anyi wa kutumia nguvu, wizi wa maungoni, wapiga debe na wavuta bangi na kikosi cha mbwa mwitu.

Akiongea na waandishi wa habari kamishna wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumekuja baada ya kufanya operesheni kali katika maeneo tofauti  jijini Dar es Salaam.

Kufuatia zoezi hilo jeshi hilo pia limekamata lita 952 za pombe aina ya gongo, bangi puli 227, kete 210 na misokoto 144 kutoka maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam.

Kikosi cha polisi cha kupambana na wizi wa simu kimewakamata watuhumiwa watatu wa makosa ya uporaji wa simu mkoa wa Kinondoni ambao ni Richard Augustino (18), Abdallah Chande (36) Abdallah Said (22) wote wakiwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY