Jeshi la Nigeria lawaachia huru watu 249 waliodhaniwa kuwa Boko Haram

0
123

Jeshi la Nigeria limewaachia huru watu 249 waliokuwa wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kuhusika na kundi la Boko Haram.

 Gazeti la Vanguard la nchi hiyo limemkariri msemaji wa jeshi hilo, Sani Usmani akikiri jeshi hilo kukosa ushahidi wa kuwatia hatiani watu hao hivyo limewaachia huru. ‘Jeshi litawapa kila mmoja $10 (wastani wa TZS 21,500) kwa kushikiliwa na jeshi.

Watu hao walioachiwa wanajumuisha wanaume 69, wanawake 46 na watoto 34 miongoni mwao wakiwemo raia wawili wa nchi jirani ya Cameroon.

Kwa mujibu wa gazeti la Vanguard, jeshi la Nigeria limekuwa likilaumiwa mara kwa mara kwa ukamataji na ushikiliaji wa watu ambao hufanyika kinyume cha sheria wakati wa shughuli zao zinazolenga kuliondoa kundi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

LEAVE A REPLY