Jeshi la Magereza kujenga kiwanda cha sukari

0
201

Jeshi la Magereza limetiliana saini na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF na NSSF ili kufufua kilimo cha miwa na kiwanda cha sukari mkoani Morogoro kitakachozalisha zaidi ya tani za sukari 30,000 kwa mwaka.

Aidha, kiwanda hicho cha sukari kitaondoa tatizo la uhaba wa sukari nchini ambalo linatokea kila mwaka sambamba na kuondoa utegemezi wa sukari ambayo huagizwa kutoka nje ya nchi wakati ambao hakuna sukari ya kutosha nchini.

Akizungumza baada ya tukio hilo Dar es Salaam jana, Mkuu wa jeshi hilo, Juma Malewa alisema Machi Mosi mwaka huu kilimo cha miwa kitaanza katika eneo la gereza Mbigiri lililopo Morogoro.

Alisema kufufuliwa kwa kilimo cha miwa na pia kiwanda hicho cha sukari kinaendana na kauli ya Rais wa awamu ya tano, John Magufuli ya kuifanya Tanzania ya viwanda.

Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Pensheni wa NSSF, Godias Kahyaara alisema kiwanda hicho kitazalisha tani 30,000 za sukari kila mwaka na kwamba tani zaidi ya 400,000 zitazalishwa katika kilimo cha miwa kwenye shamba hilo linalomilikiwa na Jeshi la Magereza.

Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio alisema kiwanda hicho kitaokoa fedha za kigeni ambazo hutumika kila mwaka kwa ajili ya kuagiza sukari nje ya nchi.

Ametoa wito kwa wakazi wa maeneo jirani na kiwanda hicho kuongeza uzalishaji wa miwa kwaajili ya kuuza kiwandani ili kuchochea uchumi wao na pia kuongeza uzalishaji wa sukari kuhakikisha kwamba hakuna sukari inayoingizwa kutoka nje ya Tanzania.

Pia asema ukarabati wa kiwanda hicho unaendelea na pia wanaendelea kusafisha mashamba ya miwa kwaajili ya kuanza kilimo Machi mosi mwaka huu.

LEAVE A REPLY