Je, Diamond na Tanasha wameachana ama ni kiki za kibiashara?

0
653

Maneno yamekuwa mengi mtaani baada ya taarifa za kuachana kwa wapenzi wawili katika ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Tanasha Donna.

Maneno hayo yameibuka baada ya Tanasha kuchapisha ujumbe katika mtandao wake wa Instagram akiwaonya wanawake wenzake kutovumilia wapenzi wanaojisikia.

Kutokana na machapisho hayo, Tanasha alitoa dalili kwamba mambo sio shwari katika uhusiano wake na msanii huyo, Diamond Platinumz.

Aliandika: Watu kama hawa hawana roho na ubinaadamu uliosalia ndani mwao. Ushetani mtupu ni kama kucheza densi na shetani. Tuwasamehe, waacheni na kumwacha Mungu kukabiliana nao.

Watu kama hao kila mara huamini kwamba majuto hayatawafikia hadi yanapowafikia. Mara nyengine unahitaji uzoefu ili kujifunza, ombeni kila siku mara tano kwa siku iwapo itawezekana. Kwasababu kukabiliana na baradhuli ni sawa na kukabiliana na shetani mwenyewe. Lindeni roho zenu, alisema Tanasha.

Kulingana na uvumi ulioenea katika baadhi ya vyombo vya habari nchini Tanzania ni kwamba mtangazaji huyo aliyebadilika na kuwa msanii alilumbana na mamake Diamond alipojaribu kuondoka Tanzania na mwanawe.

”Mungu huwaondoa watu fulani katika maisha yako kwasababu alisikia mazungumzo ambayo hakuyasikia na kuona vitu ambavyo hukuviona”…alichapisha.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao pia wamedai kwamba Tanasha alimuondoa baba wa mwanawe, dadake na mamake miongoni mwa wafuasi wake katika mtandao wa Instagram.

Lakini cha kushangaza ni kwamba malalamishi yaliochapishwa na Tanasha yanajiri chini ya wiki mbili baada ya wawili hao kutoa kibao cha ushirikiano kwa jina Gere.

Katika kibao hicho kilichotazamwa na zaidi ya watu milioni tano, wawili hao wanaonekana wakiwazomea wale wanaoonea wivu uhusiano wao huku Tanasha akimwambia mpenzi wake kutomdanganya.

Wawili hao hata hivyo hawajaucheza wimbo huo kwa pamoja katika majukwaa na wengi wanahisi kwamba huenda Diamond na Donna wanatumia kiki ya ‘kuachana kwao’ ili kuweza kuuza muziki huo zaidi.

LEAVE A REPLY