Jaydee: Sina mpango wa kuanzisha lebo

0
40

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee amefunguka na kusema kuwa hana mpango wa kufungua rekodi lebo ila atawasaidia wasanii wachanga kwa namna nyingine.

Lady Jay Dee ambaye jina lake kamili ni Jiudith Wambura amesema kuwa hajawahi kuwa na record label kwasababu si kila msanii lazima awe na record label kwani unaweza kumsaidia msanii kwa kufanya nae kolabo bila kumchaji.

Pia Jide amesema kuwa amekuwa akifanya vizuri na zake zinakubalika kwasababu anajiamini na nidhamu kwenye kazi.

Jide amesema kuwa “Nimekuwa nikifanya vizuri na kazi zangu zinakubalika kwa sababu ya ‘consistence’ na ‘discipline’ kwenye kazi, naipenda sana kazi yangu ndiyo maana nafanya vizuri.

Ameongeza kwa kusema kuwa “Kazi zote ninazoletewa kwa ajili ya kushirikishwa ninazipenda kwa sababu kabla ya kushiriki katka kazi na msanii yeyote lazima niwe nimeisikiliza na nimeipenda ndipo nafanya maamuzi ya kushirikiana naye.

Mwisho amemalizia kusema kuwa “Mambo yamebadilika, watu wengi wapo kwenye social media, mtu anaweza kuimba akaposti mitandaoni wakamuona, si lazima akashindane sehemu.

LEAVE A REPLY