Jay Moe atoa tahadhari ya ‘fake version ya NISAIDIE KUSHARE’

0
333

Rapa mkongwe na mmoja wa waasisi wa kundi la WATEULE, Juma Mohamed Mchopanga a.k.a Jay Moe ametoka tahadhari kwa redio za nchini kutocheza audio ya ngoma yake mpya ya NISAIDIE KUSHARE.

Jay Moe amedai kuwa redio yoyote itakayoicheza ngoma hiyo kwa sasa itakuwa inacheza ngoma FEKI kwasababu ni lazima itakuwa imetengenezwa kutoka katika version ya video.

Jay Moe ametoa maelekezo kuwa bado hajaachia audio version ya ngoma hiyo maalum kwaajili ya redio.

Moe amedai kuwa kwenye audio ya ngoma hiyo hakutokuwa na baadhi ya sauti zinazosikika kwenye video ya ngoma hiyo hivyo ni vyema redio za nchini zikafanya subira kuingojea orijino version ya ngoma hiyo.

Wasanii wengine kuiga staili hii?

LEAVE A REPLY