Jay Dee kuachia albam mpya mwaka huu

0
69

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee amefunguka na kusema kuwa anatarajia kuachia albam mpya itakayokwenda kwa jina la 20.

Jay Dee amesema kuwa ameamua kuita albam yake jina hilo kwasababu ana miaka 20 kwenye muziki wa Bongo Fleva hadi leo.

Mwanamuziki huyo ameitaja namba 20 kama ndiyo namba yake ya bahati, kwani anatarajia kuachia Album yake ya nane na jina la Album hiyo itaitwa 20.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter “Album yangu ya nane itaitwa 20, hii ni kutokana na kwamba itatoka mwaka huu 2020 ambapo naadhimisha miaka 20 kwenye kiwanda cha muziki, pia Album hii itakua na jumla ya nyimbo 20″.

Sababu ya ya Album hiyo kuitwa jina la 20 ni kutokana na yeye kukaa kwenye game kwa miaka 20 tangu mwaka 2000, pia ndani ya Album hiyo kutakuwa na jumla ya nyimbo 20.

LEAVE A REPLY