Japan yatuma kikosi cha ‘mapambano’ Sudani Kusini

0
232

Kundi la wanajeshi wa Japan limewasili nchini Sudan Kusini kwaajili ya kuanza jukumu la kulinda amani nchini humo.

Kundi hilo la wanajeshi lililopewa mamlaka ya kutumia nguvu pale inapohitajika linakuwa la kwanza ‘endapo litapambana’ kupigana nje ya Japan tangu kuisha kwa vita kuu ya pili ya dunia.

Wanajeshi hao wapatao 350 litachukua nafasi ya wanajeshi wengine wa nchi hiyo ambao walikuwa kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo lakini kikiwa na katazo la kutumia nguvu.

Kikosi kipya kitakuwa na jukumu la uhandisi na ujenzi kwenye mji mkuu wa Sudani Kusini, Juba.

Nchi ya Kenya iliviondoa vikosi vyake nchini Sudan Kusini kufuatia kutimuliwa kazi kwa Luteni Jenerali Ndiek wa nchi hiyo kufuatia repot maalum ya waangalizi wa Umoja wa Mataifa kudai kuwa alishindwa kutekeleza majukumu ya kusimamia na kulinda usalama wa raia wa Sudani Kusini kwa ufanisi.

LEAVE A REPLY