Japan: Kimbunga Mindulle chavunja safari za ndege 387

0
99

Mamlaka za Japan zimeamua kusitisha safari zote za anga nchi humo kufuatia kimbunga chenye nguvu cha Mindulle kuelekea kwenye mji mkuu wan chi hiyo, Tokyo.

Karibu ndege 400 zimeamriwa kutua kutokana na mvua kubwa na upepo mkali.

Kimbunga cha Mindulle kinatarajiwa kusababisha mkatiko mkubwa wa ardhi kufikia baadae leo huku kikielekea upande wa kaskazini kwenye mji wa Tohoku kutoka mji wa Tokyo.

Kimbunga hicho kinatarajiwa kusababisha upepo wa kasi ya 180km kwa saa.

Mamlaka ya hali ya hewa ya Japan imetoa tahadhari kwa mji wa Tokyo kwa kuwaambia wakazi wajiandae na maporomoko ya ardhi, mafuriko kwenye maeneo ya bondeni, mito kutapika maji pamoja na upepo mkali.

Kimbunga hicho kimesababisha mashirika ya ndege kusitisha safari za ndege zipatazo 387 ambazo zilikuwa zilikuwa zinatoka kwenye uwanja wa ndege wa Haneda uliopo mjini Tokyo.

Zaidi ya abiria wa ndani ya Japan 26,910 wameathiriwa na kufutwa kwa safari 145 za ndege za shirika la ndege la Japan Airlines wakati All Nippon Airways imefuta safari za ndani 96 na kuathiri wasafiri 21,300.

LEAVE A REPLY