Janet Jackson ajifungua mtoto wa kiume akiwa na miaka 50

0
346

Staa wa muziki wa Pop wa Marekani, Janet Jackson amefanikiwa kujifungua salama mtoto wa kiume na kuingia kwenye historia ya kuwa mmoja wa wasanii wakubwa waliojifungua wakiwa na umri mkubwa.

Janet mwenye miaka 50 amepata mtoto huyo wa kwanza akiwa na mume wake mfanyabiashara wa Qatari, Wissam Al Mana.

Licha ya umri wake kuwa mkubwa lakini ripoti zimedai kuwa Janet amefanikiwa kujifungua bila vikwazo.

Tetesi za ujauzito wake zilianza kutapakaa mwezi Aprili kufuatia kusitisha ziara yake ya muziki ya UNBREAKABLE TOUR kwa kile alichokieleza kuwa ni kupanga masuala ya kifamilia.

Janet Jackson alifunga ndoa na mumewe mwaka 2012.

LEAVE A REPLY