Janet Jackson afunguka furaha yake baada ya kupata mtoto

0
429

Mwanamuziki wa Marekani, Janet Jackson amesema kuwa kwasasa anafuraha sana baada ya kupata mtoto.

Janet aweka wazi namna alivyokuwa akihangaika kuipata furaha yake, anasema alikata tamaa kirahisi lakini alifurahi sana baada ya kuwa mama.

Mwanamuziki huyo wa miondoko ya pop amesema alikuwa akikabiliwa na msongo mkubwa wa mawazo maisha yake yote kwa kukosa mtoto.

Mwanamama huyu mwenye miaka 52 alimshukuru Mungu baada ya kupata mtoto wake wa kiume.

Jackson ni mmoja kati ya waimbaji wenye mafanikio katika historia ya chati za muziki za Marekani, akiwa na nyimbo 27 ambazo zilikua miongoni mwa nyimbo 10 bora na nyingine 10 zilizokamata namba moja zikiwemo nyimbo kama Nasty,That’s The Way Love Goes na Again.

Alizungumzia namna alivyokuwa akipambana na msongo wa mawazo wakati huo alikuwa anaandaa albamu ya mwaka 1997 , The Velvet Rope, ambayo iliandikwa akiwa katika hali ya kuchoka kihisia

Katika kitabu chake alichokichapa mwaka 2011, True You, nyota huyo alisema alihisi kutojiamini tangu akiwa mtoto-alipokuwa akifanya kazi katika Televisheni, akiwa na miaka 10.

LEAVE A REPLY