Jambazi sugu raia wa Burundi auawa Dar

0
116

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limewauwa majambazi watatu akiwemo raia wa Burundi ambao walikuwa wakifanya uhalifu katika maeneo mbalimbali  ya jiji hilo na nchini kwa ujumla.

Hayo yameelezwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ambapo amesema kuwa katika majambazi hao watatu waliouwawa kwenye oparesheni maalum ya jeshi hilo, iliyofanyika kuanzia Novemba 11 hadi 30, 2017 alikuwepo raia mmoja wa Burundi aliyejulikana kwa jina la Fanueli Luchunda Kamana ambaye ana mafunzo ya kijeshi na kufikia ngazi ya Komando.

Aidha Mambosasa ameeleza kuwa raia huyo wa Burundi ndio alikuwa kiongozi wa kundi hilo ambapo alikuwa anakwenda Burundi kila baada ya kufanya tukio.

Pia amesema kuwa baada ya kwenda kuonesha silaha walizokuwa wameficha katika eneo jingine, Mburundi huyo alimvamia askari kwa lengo la kumshambulia ili wajinasue.

Kamanda Mambosasa amesema kuwa “Baada ya kumvamia askari wetu majambazi wale wawili walianza kukimbia lakini askari wetu walifanikiwa kuwadhibiti kwa kuwafyatulia risasi na baadae kuwafikisha katika hospitali ya Mwananyamala ambapo walibainika kuwa wamefariki”.

LEAVE A REPLY