Jaffo: Serikali itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha vita dhidi ya mafisadi inafanikiwa

0
84

Serikali imesema kuwa itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha vita dhidi ya mafisadi inafanikiwa kwani kuna kila dalili kuwa vita hiyo wataishinda kutokana na kuanzishwa kwa mahakama maalumu ya ufisadi.

Kauli hiyo imesemwa na naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Jaffo wakati akifungua mkutano uliowahusisha watumishi wa umma kutoka wizara mbali mbali na mashirika ya umma uliofanyika wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Waziri huyo amesema kuwa serikali ina nia nzuri ya kupambana na ufisadi ili kuleta maendeleo kwa jamii kwani mafisadi wamekuwa wakikwamisha shughuli za serikali kwa wananchi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa mafunzo kutoka taasisi isiyokuwa ya serikali inayojishughulisha na uchunguzi dhidi ya ufisadi, Shakibu Nsekela amesema kuwa kuna haja ya kuanzishwa vitengo vya uchunguzi wa rushwa katika taasisi za umma.

LEAVE A REPLY