Jacqueline Wolper: Siwezi kutoka kimapenzi na mwanaume wa mtu

0
315

Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amefunguka na kusema hawezi kutoka kimapenzi na wanaume ambao wameoa kwa madai anahofia wanaweza wakatelekeza familia zao kwa maana yeye akichukua kitu huwa hawi lelemama hata kidogo.

Wolper amesema kuwa amekuwa muoga sana kufanya jambo hilo kwa kuwa anaogopa laana kutoka watu wazima.

Pamoja na hayo, Wolper ameendela kwa kufafanua baadhi ya mambo kwa kusema “No siongelei umri hapa naongelea imani, kwa sababu mimi nikimchukua mume wa mtu sitokuwa lele mama halafu sasa kule nyumbani kwake atakuwa anapunguza mapenzi kwa hiyo kidogo nakuwa na huruma na ndiyo maana mimi nataka niwe na cha kwangu sitaki kuiba cha mtu”.

Katika siku za hivi karibuni Jacqueline Wolper amekuwa akiandamwa sana katika skendo la kutoka na wanaume wadogo kiumri japo yeye mwenyewe amekuwa mgumu kuweka bayana kuhusiana na mambo hayo ambayo wanazungumziwa mtaani.

 

LEAVE A REPLY