Jacqueline Wolper kutosapoti kazi za Harmonize kisa Sarah

0
418

Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa hawezi hataweza kukaa na kusapoti kazi za Harmonize sababu anamuonea huruma mpenzi wake Sarah.

Siku chache zilizopita Wolper na mpenzi wa Harmonize Sarah walirushiana maneno kwenye Instagram baada ya Wolper kudaiwa kumtumia mesejei Harmonize jambo ambalo Wolper amelipinga.

Ambapo Sarah alimtaka Wolper aache kumtumia Meseji za kumtaka Mpenzi wake Harmonize jambo ambalo lilinkera Wolper kwani aliweka wazi kuwa akaunti yake ya Instagram ilidukuliwa hivyo hakuwa yeye aliyekuwa anatuma Meseji.

Wolper amesema kuwa ameamua kuacha kabisa kusapoti kazi za Harmonize kwasababu hakifanya hivyo mpenzi wake anajua anataka warudiane.

Wolper amesisitiza kuwa amefikia uamuzi wa kumblock Harmonize na Sarah kwenye Instagram ili aepushe maneno maneno.

LEAVE A REPLY