Jacqueline Wolper atamani kupata mtoto

0
81

Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper ameibuka na kusema katika vitu anatamani mwaka huu ni kupata mtoto  wake  wa kwanza.

Wolper ambaye amethibitisha kuwa kwenye mahusiano na mwanaume ambaye amesisitiza kuwa  hataweza kumuweka hadharani Lakini amesema huu mwaka anatamani kupata mtoto bila kujali kama itakuwa ndani ya ndoa au nje.

Wolper alisema anaamini mwaka huu kwake utakuwa na neema kubwa, ikiwemo kujaaliwa mtoto kama ambavyo amekuwa akitamani iwe hivyo.

Nina mipango mingi sana kwa mwaka huu, unajua kila unapoweka mikakati yako mwanzoni mwa mwaka ndio nafasi nzuri ya kufanya mambo yako kwa umakini zaidi, kwa sasa ninachowaza ni mtoto”.

Wolper ambaye amewahi kuwa muwazi sana kwenye Suala la mahusiano katika siku za nyuma amesema hawezi kufanya hivyo kwa sasa kwani Mitandao ndio iliyoua mahusiano hapo nyuma.

LEAVE A REPLY