Jacqueline Wolper apagawa na penzi la Rich Mitindo

0
43

Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amesema kuwa, yupo tayari aonekane chizi baada ya kuzimikia penzi la Rich Mitindo.

Wolper amesema kuwa watu wengi wanamuona kama chizi kwenye penzi hilo, kwani amejitosa moja kwa moja huku akiwa haambiliki wala hasikii la mtu.

“Acha waniite chizi, lakini ukweli ni kwamba, sasa hivi nimenasa kwenye huba la kweli nililolitafuta siku nyingi sana na sikuwahi kulipata,” anasema Wolper ambaye huko nyuma, hakuweza kudumu kwenye penzi kama ilivyo sasa kwa Rich Mitindo.

Muigizaji huyo wa Bongo Movie amekuwa kwenye mahusiano mengi lakini mwenyewe anasema kuwa penzi la Rich Mitindo limemdatisha kiasi cha kupagawa kabisa.

Wolper aliwahi kutoka kimpanzi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize wakati anaanza muziki katika lebo ya WCB chini ya  Diamond Platnumz.

LEAVE A REPLY