Jackline Wolper awataka wanawake kujishughulisha

0
377

Muigizaji wa Bongo Movie, Jackline Wolper amewataka wasichana kujishughulisha ili kujipatia kipato chao na hatimaye waweze kuheshimika katika jamii.

Jackline Wolper amesema ni wakati sasa mabinti kuacha kutegemea pesa wanazopewa na wanaume, na badala yake wajishughulishe ili kutengeneza pesa yako mwenyewe.

Amesema kuwa “Wadogo zangu wa kike 2018 mi ntaendelea kuwatia hasira, na kuendelea kuwaambia kwamba hela ya mwanaume sio ya kwako, ukishachukua hela ya mwanaume fanya kitu chako, iwe hela yako, usikubali kunyanyasika, kwa hela ya mtu, kwa hiyo wadogo zangu nitaendelea kuwaisipire ili mfanye kazi ili utambe na hela yako, usitambe kwa hela ya kuhongwa’.

Hivi sasa Wolper anamiliki biashara yake ya mavazi ambayo ana buni na kushona mwenyewe, ambayo aliwahi kusikika akisema inamuingizia pesa nyingi ingawa watu wengi wakimdharau kwa kumuita ‘fundi cherehani’.

LEAVE A REPLY