Jackline Wolper apinga Nisha kutembea na Brown

0
237

Muigizaji wa Bongo Movie, Jackline Wolper amepinga vikali taarifa za aliyekuwa mpenzi wake Brown kutoka kimapenzi na muigizaji mwenzie, Salma Jabbu maarufu kama Nisha.

Wolper amesema kuwa si kweli taarifa hizo kwani asilimia kubwa ya muigizaji huyo ni muongo sana kwa hiyo habari anazosambaza hazina ukweli wowote.


Pia Wolper amesema Nisha ni mchekeshaji hivyo haamini kabisa kama anaweza kutoka na mwanamitindo huyo na pia anazijua aina za wanawake wanaoweza kutembea na Brown haifanani kabisa na Nisha.

Wolper amefunguka hayo wakati wa kuitambulisha project yao iliyotangazwa na waigizaji wa Bongo Movie nchini.

Aidha, amesema Project yao mpya ya kijana amka itawasaidia vijana wengi waliokata tamaa ili waweze kuamka na kujikwamua kimaisha kupitia vipaji vyao hata kama ni vipaji vya wanavyodharaulika.

LEAVE A REPLY