Iyanya aachana na lebo ya Mavin Records

0
138

Mwanamuziki wa Nigeria, Iyanya amethibitisha kutokuwa tena chini ya lebo ya Mavin Records inayosimamiwa na mwanamuziki Don Jazzy.

Iyanya ameeleza kuwa kwa sasa hayupo tena katika lebo hiyo na hakuna mgogoro uliopo kati yake na Don Jazzy.

Iyanya amesema kuwa kwasasa amesaini lebo ya Temple Music lakini Mavin record ni nyumbani kwake na ataendelea kuipenda kwani hakunu bifu kati yao ila sasa ni muda wa kuelekea lebo nyingine.

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na ngoma yake mpya iitwayo Good vibe aliyowashirikisha Team Salut kutokea Uingereza.

Mavin ni lebo inayosimamia wanamuziki nyota nchini Nigeria akiwemo Tiwa Savage, Koledo Bello, Dija na wengineo.

LEAVE A REPLY