Isha Mashauzi akanusha kuacha kuimba taarab

0
53

Msanii wa muziki wa taarab nchini, Isha Mashauzi amekanusha tetesi zinazosema kwamba ameachana na taarab na badala yake amehamia katika muziki wa Bongo Fleva.

Tetesi hizo zimeanza kuenea baada ya mwanamuziki huyo kushirikishwa kwenye wimbo wa Bam Bam wa Fid Q, Richi Mavoko na Big Jaman.

Isha amesema hawezi kuacha kuimba muziki wa taarabu kwa kuwa muziki wa taarabu ndo umemtangaza na kumfanya yeye kuwa na jina alilonalo hivi sasa akisema kuwa kwa upande wa Bongo Fleva kuna wanaofanya vizuri hivyo inabidi awaachie nafasi na sio kwamba anaogopa kushindwa.

Hata hivyo Isha ameendelea kusema kwamba, “haikuwa rahisi kujiamini kufanya kazi ya Fid Q kwa kuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza kufanya wimbo wa Bongo Fleva, nilikuwa nahofia japo niliingiza yale mashairi kwa siku moja na kwa muda mfupi kama masaa mawili hivi nikayaacha studio na kuamini chochote kitakacho tokea nitapigiwa simu”.

Pia Isha amemaliza kwa kusema anapenda kujifunza pale anapokosea na hapendi kiki kwa kuwa anaamini kwamba muziki wake pekee ni kiki tosha hivyo hawezi kutafuta kiki na kama kuna nyimbo yake ambayo anaambiwa ameimba vibaya huwa anakaa na kuisikiliza ili kuweza kuifanyia marekebisho badae.

LEAVE A REPLY