IS yapewa saa 48 kuondoka Syria

0
168

Wapiganaji wanaoungwa mkono na jeshi la Marekani nchini Syria limewapa saa 48 wapiganaji wa kundi la Islamic State of Iraq and the Levant (ISIL) kuondoka kwenye ngome yao kuu iliyopo kwenye mji wa Manbij nchin Syria.

Kauli hiyo ya wapiganaji hao imekuja siku mbili tu baada ya kutolewa taarifa ya majeshi yanayoongozwa na Marekani kwenye mapambano ya kundi la IS kuua makumi ya raia kwenye eneo la Tokhar kaskazini mwa mji wa Manbij.

Baraza la kijeshi la Manbij ambalo ni sehemu ya majeshi ya Syria (SDF) yalitoa onyo hilo siku ya jana.

Pamoja na onyo hilo SDF na muungano wa wapiganaji wa kiarabu na kikurdi wanaoungwa mkono na Marekani pia wamewatahadharisha raia kuondoka au kukaa mbali na maeneo yanayotarajiwa kushambuliwa.

‘Tunachukua hatua hii baada ya ISIL kuwatumia wakazi wa eneo hili kuwa ngao, pia baada ya vyombo vya habari kutushambulia na kulinda kila kitu ambacho raia wamekiacha nyuma yao’ amesema mmoja wa makamanda wa SDF.

Jeshi hilo la washirika bado linachunguza ukweli wa idadi kamili ya raia waliofariki kufuatia shambulio la anga lililofanywa na majeshi hayo siku ya Jumanne ambapo taasisi mbili ziliripoti idadi inayokinzana ya watu waliofariki.

LEAVE A REPLY