Irene Uwoya hawaomba radhi waandishi wa habari

0
355

Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya amewaomba radhi waandishi wa habari  kwa kitendo chake cha kuwarushia pesa wakiwa katika mkutano na wanahabari hao.

Uwoya amesema kuwa hakufanya hivyo kwa lengo la kuwadhalilisha kama ilivyotafsiriwa na amesisitiza kuwa alifanya kwa moyo mzuri kutokana na juhudi za waandishi wa habari kwenye kusambaza taarifa.

Uwoya alifanya hivyo akiongea na waandishi wa habari waliojitokeza katika ukumbi wa Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam jana Julai 15, 2019 kwenye mkutano ulioitishwa na wasanii wa Bongo Muvi ukiwa na lengo la kuzungumzia uzinduzi wa Swahiliflix ambao ni mtandao wa kuuzia muvi, unaotarajiwa kufanyika tarehe 31, mwezi huu mwishoni.

Alichokisema:- Ndugu zangu waandishi wa habari, leo katika press conference ya Swahili Inflix na ndugu zetu waandishi wa habari niliamua kutoa fedha kwa style ya kutunza.

Baadhi yenu mmekwazika kwa kitendo hicho nawaomba radhi sana sikuwa na nia mbaya juu yenu, binafsi nawapenda waandishi wa habari kwani nyie ni watu muhimu sana katika jamii.

Sikufanya hivyo kwa lengo la kuwadhalilisha kama ilivyotafsiriwa.Kama binadamu moyo wangu ulijawa na upendo na furaha iliyopitiliza ndipo niliona niweze kushiriki nanyi furaha hiyo kwa aina ile ya kuwatunza pesa,sababu mara nyingi mmekuwa watu muhimu katika kazi na mambo yote yanayohusu sanaa yetu na jamii kwa ujumla.

Baadhi ya waandishi ambao kwa bahati mbaya waliharibu vifaa vyao wakati wa kuokota shukrani yangu hiyo(pesa) naomba mniwie radhi na mnisamehe sana na poleni sana kwa changamoto.

LEAVE A REPLY