Irene Uwoya akanusha kutoka kimapenzi na Kayumba

0
248

Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya amekanusha taarifa zinazosambaa mtandaoni kuwa anatoka kimapenzi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Kayumba.

Kauli ya muigizaji huyo imekuja baada ya kutokea maneno katika mitandao ya kijamii kuwa kwasasa anatoka na Irene Uwoya baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake Dogo Janja.

Uwoya amesema kuwa taarifa hizo hazikuwa ukweli wowote ila watu wanaamua kumchafua ila hana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki huyo isipokuwa ni urafiki wa kawaida tu.

Pia Uwoya amesema mashabiki wake wawe wapole kama wanataka kumjua shemeji yao watamjua lakini siyo Kayumba wanayomsema.

“Nina-chojua ni kwamba watu wengi wako ‘bize’ kujua mimi niko na nani hakuna mtu ambaye watamuacha kumtaja kwenye listi zao kuwa natoka naye kimapenzi hivyo siwasha-ngai na kingine siwezi kutoka na Kayumba wajue hilo’.

Irene amesema kuwa watu wanataka kujua kwasasa anatoka na nani ndiyo mana kila matu wanamtaja kuwa anatoka nae kimapenzi baada ya kuacha na Dogo Janja.

LEAVE A REPLY