Irene Uwoya aikataa ndoa

0
60

Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hayupo tayari kuingia kwenye ndoa kwa sababu bado anakula ujana.

Uwoya amedai kuwa wanawake wengi wanaingia kwenye ndoa ikiwa bado hawajamaliza mambo ya ujana kitu kinachopelekea ndoa zao kuyumba.

Amesema kuwa wanawake wengi wanakimbilia kwenye ndoa mapema, lakini baada ya muda ndoa inavunjika maana bado wanatamani sana mambo ya nje na kusahau ndoa.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa kutokana na hayo mejifunza sana hivyo kwa sasa anakula kwanza ujana mpaka atosheke, halafu ili akishaingia kwenye ndoa atakaa kwa kutulia.

Irene Uwoya amewahi kufunga ndoa mbili kipindi cha nyuma na zote zimevunjika moja ikiwa na msani wa Bongo Fleva, Dogo Janja.

LEAVE A REPLY