Irene Uwoya afunguka mahusiano yake na Dogo Janja

0
243

Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya amefunguka na kusema kuwa Dogo Janja aliwahi kuchepuka kwenye ndoa yake kwa kutembea na mwanamke mwingine.

Kauli ya muigizaji huyo imekuja baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa ndoa ya wawili hao imevunjika rasmi.

Irene amefunguka kuhusiana na maisha yake lakini haswa kuhusiana na yale yanayoendelea kuenea kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na ile kinachosemekana ameachana na Dogo Janja.

Muigizaji huyo amesema kuwa taarifa za yeye kuachana na Dogo Janja zimeanza kuzagaa baada ya kuonekana akiwa nchini Dubai akila bata na mwanaume mwingine jambo ambalo limezua gumzo katika mitandao ya kijamii.

Irene amesema kuwa kwa upande wake hakuna tatizo kwa kuwa anaendaga nje ya nchi kwa ajili ya kazi zake za Sanaa tofauti na watu wanavyohisi kuwa anaendaga nchi za nje kwa ajili ya kukutana na wanaume wengine.

Pia muigizaji huyo ameongezea kwa kusema kuwa hajaachana na mume wake huyo Dogo Janja kama taarifa zinavyosambazwa katika mitandao ya kijamii.

LEAVE A REPLY