Irene Uwoya achukizwa na matusi ya mashabiki mitandaoni

0
310

Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Irene Uwoya amechikizwa na baadhi ya tabi ya mashabiki wao ambao wanawatukana katika mitandao ya kijana.

Irene Uwoya amefunguka kwa kusema kuwa anachukizwa na tabia hizo za baadhi ya mashabiki waliopo mitandaoni kushindwa kutoa ushauri kistaarabu na badala yake kuanza kuwashambulia kwa kuwatukana.

Uwoya ameeleza hayo baada zile kelele za wasanii wengine kudai mashabiki zao ndiyo wamekuwa vinara katika kuwakosoa pindi wanapokuwa wame-post kazi zao hata muda mwingine maisha yao binafsi wakiwa sehemu wana-enjoy na marafiki zao.

Muigizaji huyo amesema kuwa mashabiki wapo katika nafasi nzuri ya kusema kama wanakosea au wanapatia lakini njia wanayoitumia kuwaelewesha siyo nzuri, wanatumia matusi badala ya kuwambia taratibu bila kutukana.

Uwoya amesema kuwa mashabiki wao wanasahau kwamba wasanii ni binadamu kama binadamu wengine wanaishi kama watu wengine.

Pia ameongeza kuwa kusema kuwa msanii siyo malaika, saa zingine hawajui mtu unakuwa katika hali gani, labda umefiwa au unaumwa wao wanatukana tu ili mradi wakutoe kwenye mood iliyonayo kwa muda huo.

LEAVE A REPLY