Irene Paul afunguka shutuma za kulinga

0
109

Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Paul amesema kuwa kitu ambacho hakipendi ni kujichanganya na watu ambao hawajui kiundani na ndiyo maana wanamuambia anaringa.

Kauli ya muigizaji huyo imekuja baada ya kuambiwa na watu kuwa anaringa sana, anajisikia ndiyo hapendi kukaa na wenzake.

Irene Paul aliyejizolea umaarufu mkubwa kutokana na uigizaji wake amefunguka na kusema kuwa yeye hayo ndiyo maisha yake aliyojichagulia lakini siyo kama anaringa wanavyosema watu wengine.

Irene amesema alijifunza kutoka kwa wazazi wake kutulia nyumbani na siyo kwenye majumba ya watu kwa sababu ya kukwepa majungu.

Pia amesema kuwa hakuna kitu ambacho anakichukia kama kujichanganya kwenye makundi ambayo anayajua mwisho wake ni mbaya katika jamii.

 

 

 

 

LEAVE A REPLY