Irene Paul afunguka sababu ya kutojichubua

0
90

Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Paul ameamua kuwahamasisha mastaa na watu mbalimbali kuepuka gharama ya kujitengeneza badala yake wanaweza kubaki na uasili wao na wakapendeza.

Kauli ya muigizaji huyo imekuja baada ya kuona baadhi ya mastaa wengi hapa mjini hupenda kutumia vipodozi.

Irene alisema amekaa na kujitathimini na kugundua kuwa hatumii gharama kubwa kununua nywele za bei mbaya au kutumia madawa ya usoni, lakini bado anaonekana mrembo.

Amesema kuwa “Ukitaka kuniangalia kuanzia kichwani hadi ngozi yangu situmii gharama hata kidogo, naamini mastaa wengine wakiamua kuwa jinsi walivyo watapendeza na wataepuka gharama ambazo si za muhimu,”.

Pia muigizaji huyo amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani hivi karibuni atawaletea mzigo mpya sokoni.

LEAVE A REPLY