Iran yaunda jeshi la ukombozi

0
330

Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa na shirika la utangazaji la AlJazeera, nchi ya Iran imeunda kikosi maalum cha jeshi ambacho imekiita ‘Jeshi la Ukombozi’ ambalo vikosi vyake vinatarajia kutumwa kwenye nchi za Kiarabu.

Hivi sasa, nchi ya Iran inashiriki kwenye kile kinachoonekana kama mgogoro wa madaraka baina ya madhehebu ya Kiislam ya Shia na Sunni kwenye mgogoro wa nchi za Syria na Yemen.

Kwa mujibu wa kauli ya Mohammad Ali Al Falaki anayeongoza askari wa kikosi cha Islamic Revolutionary Guard Corps  iliyochapishwa na Al Mashriq, Iran inapambana kwenye vita za sehemu tatu: Iraq, Syria na Yemen.

Iran ‘imetengeneza Liberation Army nchini Syria chini ya uongozi wa Qassem Soleimani’ amesema Falaki, anayeongoza vikosi hivyo nchini Syria.

Bado haijajulikana jeshi hilo ni kubwa kiasi gani. It was not clear how large the Liberation Army would be.

‘Vikosi vinavyounda jeshi hili sio vya wanajeshi wa Iran peke yake. Kwenye kila eneo ambapo kuna mapigano tunatengeneza jeshi kutokana na watu wa hapo na kuwasaidia’

Mwezi Januari shirika la Al Jazeera liliripoti kuwa nchi ya Iran inawadahili maelfu ya wapiganaji wa Afghanistan ambao ni wafuasi wa dhehebu la Shia ili kuweka jitihada zao kwenye vita inayoendela nchini Syria.

 

LEAVE A REPLY