Iran yapiga marufuku Game ya ‘Clash of Clans’

0
145

Tume maalum ya Serikali ya Iran imetaka kuwekwe udhibiti maalum kutokana na ripoti za wanasaikolojia kudai kuwa mchezo ‘Game’ ya ‘CLASH OF CLANS inahamasisha vurugu na ugomvi baina ya makabila.

Pia ripoti za wanasaikolojia wanaochunga sera za teknolojia wamedai kuwa mchezo huo unaweza kuharibu maisha ya familia iwapo vijana wadogo watauendekeza.

Takeimu zilizokusanywa mapema mwaka huu zinaonyesha kuwa zaidi ya 64% ya wacheza game nchini Iran huwa wanacheza Clash of Clans.

Uamuzi wa kudhibiti Game hiyo umeanza kutekelezwa tarehe 27 Disemba huku baadhi ya wachezaji wakilalamikia kushindwa kucheza Game hiyo mtandaoni.

Iran pia imezuia uchezwaji wa Game ya Pokemon Go.

LEAVE A REPLY