Instagram yaifuta picha ya utupu ya Amber Rose

0
575

Baada ya mwanamitindo wa Marekani, Amber Rose kutupia picha yake ya utupu katika mtandao wa Instagram, hatimaye mtandao huo imefuta picha hiyo.

Mtandao huo imefuta picha hiyo baada ya gumzo kuenea kwenye mtandao huo duniani kutokana na picha hiyo chafu iliyowekwa na mwanamitindo huyo.

Mtandao huyo wa kijamii wa Instagram una watumiaji zaidi ya milioni 500 duniani kote umeamua kuitoa picha hiyo ili kusitisha marumbano kwenye mtandao.

Picha hiyo ambayo Amber aliiweka kwenye mtandao huo, ilifutwa kutokana na kukosa maadili.

Hii ndiyo picha ya Amber Rose aliyoiweka kwenye mtandao wa kijamii
Hii ndiyo picha ya Amber Rose aliyoiweka kwenye mtandao wa kijamii

Mara nyingi mtandao huo huziondoa picha ambazo zinaripotiwa kutokuwa na maadili katika jamii.

Baada ya kufutwa picha hiyo ya utupu ambayo imewatoa udenda vidume wengi mitandaoni, Amber ameandika ujumbe mwingine kwenye mtandao huo unaoonyesha masikitiko yake baada ya kufutiwa picha hiyo huku mashabiki wakimuunga mkono kwa kitendo hicho.

LEAVE A REPLY