Indonesia kuwanyonga watu 14 kwa makosa ya dawa za kulevya

0
140
Serikali ya Indonesia imesisitiza kuwa itatatekeleza adhabu ya kifo kwa wafungwa 14 wa makosa yanayohusiana na dawa za kulevya waliohukumiwa adhabu hiyo licha ya tahadhari kutoka kwa Umoja wa Mataifa.
Kamishna wa Umoja wa mataifa wa haki za binadamu Zeid Ra’ad al-Hussein ameelezea kutoridhishwa kwao na serikali ya Indonesia kutekeleza adhabu hiyo waliyoiita ‘isiyohaki’ na kuitaka serikali ya Jakarta kuikomesha adhabu hiyo.
Wafungwa wanaotarajia kukumbwa na adhabu hiyo bado hawajatajwa lakizi inadhaniwa kuwa ni raia kutoka wanatokea nchi za Nigeria, Zimbabwe, Pakistan and India.
Endapo adhabu hiyo itatekelezwa, wafungwa hao wanatarajia kunyongwa kwenye gereza la Nusakambangan.
Tayari wafungwa hao wameshataarifiwa kuhusu hukumu hiyo kama sheria ya Indonesia inavyotaka na huenda wakatumikia adhabu hiyo kabla ya wiki ijayo.
Mwanasheria mkuu wa serikali ya Indonesia, Muhammad Prasetyo amesema kuwa wafungwa hao tayari wameshatengwa na watanyongwa baina ya Ijumaa na Jumapili.
Bw. Hussein amesema, ‘Ongezeko la matumizi ya adhabu ya kifo nchini Indonesia inatia wasiwasi mkubwa na ninaitaka serikali ya nchi hiyo kukomesha mara moja matumizi ya adhabu hii kwasababu sio haki na haiendani na haki za binadamu’
Indonesia ni nchi yenye baadhi ya sheria kali zaidi za dawa za kulevya na mwaka jana iliwanyonga watu 14 hali ambayo ililaaniwa na mashirika ya kimataifa.

LEAVE A REPLY