IGP Sirro ateua mrithi wake kanda maalum ya Dar es Salaam

0
354

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Lazaro Mambosasa kuwa kamanda mkuu wa kanda maalum ya Dar es Salaam.

Kabla ya kuteuliwa nafasi hiyo Kamanda Mambosasa alikuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma.

Kutokana na uteuzi huo, aliyekuwa kaimu kamanda mkoa wa Dar es Salaam anakuwa kamanda wa mkoa wa Mtwara huku aliyekuwa kamanda wa mkoa wa Mtwara anapelekwa makao makuu.

Pia kamanda Sirro amemteua kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi wa Temeke, Gilles Mroto kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma akichukua nafasi ya Mambosasa aliyeteuliwa kuwa kamanda wa Dar es Salaam.

Vile vile Kamanda Sirro amemteua Emmanuel Lukula kuwa kamanda Polisi mkoa wa kipolisi wa Temeke akichuka nafasi ya Mroto aliyeteuliwa kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma.

LEAVE A REPLY